Viongozi wa Tharaka Nithi watishia kung'atuka Jubilee
- Gavana wa Tharaka Nithi Muthomi Njuki amesema kuwa kaunti yake haitamuunga mkono rais Uhuru Kenyatta na naibu wake iwapo hawateua mawaziri kutoka kaunti yake
- Njuki alisema kuwa anazungumza kwa niaba ya wananchi waliomchagua na hajutii kutoa matamshi hayo
Gavana wa Tharaka Nithi Muthomi Njuki ametishia kutounga mkono serikali ya Jubilee iwapo Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake hawatapeana nafasi za uwaziri kwa viongozi kutoka kwa kaunti yake.
Habari Nyingine: Tunataka Jubilee kukubali kuwa haikushinda uchaguzi-Raila Odinga

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Akizungumza kwenye mkutano katika makao makuu ya kaunti huko Kathwana Jumatatu Februari 13,Njuki alisema kuwa analalama kwa niaba ya wananchi na hajutia matamshi yake
" Hebu na rais afahamu kwamba bado tunamtizama tu anapowateua makatibu wakuu na mabalozi bila ya kumteua hata mmoja kutoka kwa kaunti yetu,"Njuki alisema.
Njuki alitishia kuwa iwapo rais hatapatiana cheo chochote cha uwaziri katika kaunti ya Tharaka Nithi, hakuna mkazi atakayeunga mkono serikali yake mwaka wa 2022.

Habari Nyingine:Bintiye mrembo kitinda mimba wake mwanamziki Gidi Gidi atua Kenya, miaka 3 baada ya kuzaliwa Ufaransa
Juma lililopita gavana Njuki na seneta wa Thara ka Nithi,Kithure Kindiki wanasemekana kutofautia vikali wakiwa kwenye mkutano katika shule ya upili ya Chiakariga kuhusiana na suala la iwapo kaunti hiyo isitishe kuunga mkono serikali ya Jubilee au la.
Kindiki alimtetea Uhuru kwa kuwarai wakazi wawe watulivu kwa sababu serikali ya Jubilee iko na mipango kabambe kwa kaunti ya Tharaka Nithi.
Habari Nyingine: Mbunge Otiendo Amollo afurahisha wengi kwa kujengea wajane nyumba
Njuki aliongezea kuwa Tharaka Nithi iko na viongozi ambao wamehitimu sana masomoni na hivyo basi hafai kuiwabagua.
" Wakazi wa Tharaka Nithi walijitokeza kwa wingi na wakampigia Uhuru kura,hivyo basi tunataka pia naye arudishe mkono," Njuki aliongezea.
Kulingana na habari za Nation,kaunti hiyo imepewa nafasi moja kwa Micheni Ntiba ambaye ni katibu mkuu wa Elimu ya juu,
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4J6g5VmraKnnpy8u7WMsJhmrJiWv6K3wGaloqyYnnq4rdOiqqGhkWK4trrGmquuo5Fit7auyKWcnmaYqbqt